VAZI LA KITENGE
Kitenge
ni miongoni mwa mavazi ya Kiafrika yenye heshima ya kipekee. Tofauti na aina
nyingine za vitambaa, kitenge kina sifa ya kuvaliwa na watu tofauti tofauti na
kuleta maana kwenye mitindo.
Katika
kuonyesha thamani yake, wabunifu wa mitindo wameenda mbele zaidi na kubuni hadi
mapambo ya kitenge. Leo hii si jambo la ajabu kuona makembe, mikoba na hata
viatu vya kitenge.
Kwa
miongo kadhaa sasa imeshuhudiwa kitenge kikivaliwa katika mitindo kadha wa
kadha. Kwa mfano magauni, makoti, blauzi na hata sketi.
Mwanadada akiwa katika vazi la kitenge na kuonekana mwenye kudumisha utamaduni wa mwafrika |
Kadri
siku zinavyozidi kwenda mitindo ya vitenge ya aina mbalimbali imekuwa
ikibuniwa. Ubunifu huu umekuwa ukiongeza zaidi thamani ya kitenge na hata
kukifanya kukubalika na kutambuliwa nje na ndani ya nchi kama vazi la Kiafrika.
Kuvaa
kitengekunatosha kabisa kuonyesha ni kwa jinsi gani unajali na kulinda
utamaduni wako
Katika
kipindi cha hivi karibu wabunifu hao walikuja na mashati ya vitenge kwa
wanawake. Na kabla ya kuyaingiza sokoni walionyesha kupitia maonyesho kadhaa yamitindo jinsi ya uvaaji wake.
Leo
hii imeweza kueleweka vizuri kuwa vazi la kitenge linaweza kutengenezwa shati
litakalovaliwa na mwanamke, katika shughuli zake za kiofisi.http://amynag.blogspot.com/2014/09/african-style-design-mishono-ya-vitenge_26.html
Kama ilivyo kwa aina nyingine ya mashati, mashati aina hii
yana utaratibu wake katika uvaaji
- Kwanza kabisa unatakiwa kujua rangi yako; Kwa kujua rangi yako itakuwa ni rahisi kwako kupata ushauri kuhusiana na rangi inayoendana na wewe.
- Elewa umbo lako: Usivae shati kwa kuwa tu umemuona mwenzio amevaa. Kabla ya kuvaa hakikisha unajiuliza maswali mawili matatu kuhusiana na umbo lako. Je, linaendana na aina ya shati ulilochagua. Ikiwa wewe ni mnene chagua shati lenye rangi ya giza lakini ikiwa una umbo jembamba si vibaya ukichagua rangi ya kuwaka.
- Oanisha shati lako na vazi la chini: Licha ya ukweli kuwa aina hii ya mashati inaendana na suruali na sketi, lakini ukweli ni kwamba si watu wote wanapendelea sururali au sketi. Hakikisha unachagua vazi linaloendana na mwili wako
.
- Chagua viatu sahihi: Ni kweli kabisa kila mtu ana viatu vyake anavyopendelea. Lakini ukiwa katika aina hii ya mashati unashauriwa kuvaa viatu vile vitakavyokuweka huru zaidi.
No comments:
Post a Comment