Friday, November 6, 2015



MADHARA YA KUTUMIA VIPODOZI VYENYE KEMIKALI

Kwa miaka mingi sasa, baadhi ya watu wamegubikwa na dhana potofu ya kwamba, kuwa mweupe ndiyo urembo .
Dhana hii imewafanya wengi waanze kutumia vipodozi vikali, bila kujali madhara ya baadaye.
Kwa mfano, hata baadhi ya wasanii, wake kwa waume, wamekuwa wakijibadili ngozi zao na tumewaona wakibadilika hatua kwa hatua.
Hata hivyo, unapohisi kuna uzuri, mara nyingi kuna kudhurika. Madhara ya awali ya vipodozi hivi, huonekana kwa mtumiaji kubabuka ngozi, kuwa na mabaka meusi au ngozi kuwa nyekundu. Lakini yapo madhara mengine mabaya zaidi ya hayo.
Kemikali hatari
Katika bidhaa hizo zinazotumika za kujichubua, kuna kemikali za aina mbili.
Kwanza ni ‘Hydroquinone’ na ya pili ni ‘Mercury’.
Hydroquinone kemikali hii ni sumu kali, ambayo hutumika kwa ajili ya kuchapisha picha na kutengeneza bidhaa za mpira.
Hutumika pia kama kisaidizi katika kutengeneza rangi za nywele.Mercury nayo ni kemikali ya sumu inayoweza kuuzwa katika maduka ya madawa tu tena bila maelekezo ya madaktari
linapokuja swala la afya zetu kwa siku hizi kumekuwa na mlipuko wa magonjwa mengi yasiyo kuwa na tiba na hii inachangiwa na vitu au vipodozi tunavyokua tunavitumia bila kujua nini chanzo chake na vina tengenezwa na nini, imefika  wakati watu k  lazima tujifunze na tuwe wasikivu sana hasa ujitabua na kuanza kutumia vipodozi asilia


MADHARA YATOKANAYO NA MATUMIZI YA VIPODOZI VYENYE VIAMBATO VYENYE SUMU
1.      BITHIONOL
athari zake.
Kupata mzio wa ngozi/allergic  na athari kwenye ngozi ikiwa itapata mwanga wa jua.

2.      HEXACHLOROPHENE
madhara/ athari
·  Inapenya kwenye ngozi na kuingia kwenye ishipa ya fahamu na kusababisha ugonjwa wa mishipa ya fahamu hasa kichwani.
·  Pia inasababisha ugonjwa wa ngozi na kuathirika kwa ngozi pindi unapokuwa kwenye mwanga wa jua.
·  Kwa watoto wachanga husababisha uhalibifu kwenye ubongo
·  Vile vile ngozi inakuwa laini na kusababisha kupata ugonjwa kama fangasi kwenye ngozi au maambukizi ya vimelea vya maradhi.



3.      ZEBAKI (MERCURY)
Madhara /Athari
·  Husababisha madhara ya ngozi, ubongo, figo na viungo, mbalimbali vya mwili
·  Zebaki inapopakwa kwenye ngozi kuweza kupenya taratibu ndani ya mwili na kusababisha sumu yake kuingia kwenye damu na kusababisha madhara mwengi mwilini.

Mama mjamzito akitumia vipodozi vyenye zebaki mtoto huathirika akiwa akiwa bado tumboni na huzaliwa akiwa na mtindio wa ubongo.
·  Husababisha ngozi kwa laini na kuwa na mabaka meusi na meupe
·  Husababisha mzio/ allergic wa ngozi na muwasho
·  Sumu iingiapo kwenye mishipa ya fahamu husababisha ugonjwa wa mishipa ya fahamu.
·  Sumu ya zebaki ikiingia mwilini kwa kiwango kikubwa husababisha madhara maka upofu, uziwi, upotevu wa fahamu wa madhara mara kwa mara.

Tuesday, November 3, 2015



Nguo Ndefu Ina Umuhimu Wake Kwa Mtoko Wa Usiku



NGUO fupi imekuwa maarufu kwa mitoko ya usiku kwa shughuli mbalimbali, na wadada wengi wamekua wakipendeza sana, lakini hata hivyo wengi wamesahau kuwa hata nguo ndefu ina umuhimu wake kiasi cha kufanya mavazi ya nguo fupi kwa usiku kama ndio utaratibu.

Ukitaka  kuchagua nguo ndefu kwa ajili ya mtoko wa usiku,  iwe ni sketi na blauzi,gauni,  suti nakadhalika, chagua yenye nakshi ambazo zitaendana na shughuli husika.

Unaweza pia kuchagua nguo ndefu ya kubana ama yenye mpasuo mrefu kidogo, na kiatu kirefu pia.

Uchaguzi wa nguo inayotakiwa kuvaliwa, kwanza  unatakiwa kuzingatia ambo mengi ikiwemo kuvaa kulingana na tukio husika, kama ni pati ya kawaida au ni kwa ajili ya sherehe fulani, uvaaji wako unatakiwa
kuzingatia rangi ya nguo na rangi ya mwili wako.

Kama wewe ni mweusi hutakiwi kuvaa nguo nyeusi kwani haitakupendeza, unashauriwa kuvaa nguo za rangi nyeupe,nyekundu, gold, bluu au njano.

 

Na kama wewe ni mweupe nguo ya rangi nyeusi au rangi nyingine itakupendeza kulingana na rangi ya ngozi yako.


Mfano wa nguo ndefu simple ya kutokea usiku

Nguo ndefu ni nzuri zaidi kama zitavaliwa kwa kiatu kirefu na kubeba wallet kubwa ama 'klatch.

Cha kuzingatia ni kuhakikisha kuwa nguo hiyo haikuletei tabu wakati wa kutembea kwani nguo ikiwa ndefu sana husababisha mvaaji kuishikilia na kuonekana wakati mwingine kama kituko, vaa nguo kulingana na umbo na hata urefu wako, nguo za wazi na ndefu hupendeza sana kama zitavaliwa
na mkufu au ushanga shingoni
.
Jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa, unakuwa na nguo maalum ya kutokea na unatunza vizuri nguo zako kwani hilo litakusaidia kuongeza umaridadi wako na kujiamini zaidi.

Lakini pia usisahau kuwa na vipuri vitakavyosaidia vazi lako. Faida ya vazi hili, si tu kupendeza na kuonekana maridadi bali  muda mwingine nguo ndefu hukufanya kuwa huru zaidi katika shughuli husika.

Monday, October 12, 2015

VAZI LA KITENGE




VAZI LA KITENGE

 Kitenge ni miongoni mwa mavazi ya Kiafrika yenye heshima ya kipekee. Tofauti na aina nyingine za vitambaa, kitenge kina sifa ya kuvaliwa na watu tofauti tofauti na kuleta maana kwenye mitindo.

Katika kuonyesha thamani yake, wabunifu wa mitindo wameenda mbele zaidi na kubuni hadi mapambo ya kitenge. Leo hii si jambo la ajabu kuona makembe, mikoba na hata viatu vya kitenge.

Kwa miongo kadhaa sasa imeshuhudiwa kitenge kikivaliwa katika mitindo kadha wa kadha. Kwa mfano magauni, makoti, blauzi na hata sketi.

Mwanadada akiwa katika vazi la kitenge na kuonekana mwenye kudumisha utamaduni wa mwafrika

Kadri siku zinavyozidi kwenda mitindo ya vitenge ya aina mbalimbali imekuwa ikibuniwa. Ubunifu huu umekuwa ukiongeza zaidi thamani ya kitenge na hata kukifanya kukubalika na kutambuliwa nje na ndani ya nchi kama vazi la Kiafrika.

Kuvaa kitengekunatosha kabisa kuonyesha ni kwa jinsi gani unajali na kulinda utamaduni wako
Katika kipindi cha hivi karibu wabunifu hao walikuja na mashati ya vitenge kwa wanawake. Na kabla ya kuyaingiza sokoni walionyesha kupitia maonyesho kadhaa yamitindo jinsi ya uvaaji wake.

Leo hii imeweza kueleweka vizuri kuwa vazi la kitenge linaweza kutengenezwa shati litakalovaliwa na mwanamke, katika shughuli zake za kiofisi.http://amynag.blogspot.com/2014/09/african-style-design-mishono-ya-vitenge_26.html

Kama ilivyo kwa aina nyingine ya mashati, mashati aina hii yana utaratibu wake katika uvaaji

  •   Kwanza kabisa unatakiwa kujua rangi yako; Kwa kujua rangi yako itakuwa ni rahisi kwako kupata ushauri kuhusiana na rangi inayoendana na wewe.


  •   Elewa umbo lako: Usivae shati kwa kuwa tu umemuona mwenzio amevaa. Kabla ya kuvaa hakikisha unajiuliza maswali mawili matatu kuhusiana na umbo lako. Je, linaendana na aina ya shati ulilochagua. Ikiwa wewe ni mnene chagua shati lenye rangi ya giza lakini ikiwa una umbo jembamba si vibaya ukichagua rangi ya kuwaka.

  • Oanisha shati lako na vazi la chini: Licha ya ukweli kuwa aina hii ya mashati inaendana na suruali na sketi, lakini ukweli ni kwamba si watu wote wanapendelea sururali au sketi. Hakikisha unachagua vazi linaloendana na mwili wako
.
  •  Chagua viatu sahihi: Ni kweli kabisa kila mtu ana viatu vyake anavyopendelea. Lakini ukiwa katika aina hii ya mashati unashauriwa kuvaa viatu vile vitakavyokuweka huru zaidi.