Friday, November 6, 2015



MADHARA YA KUTUMIA VIPODOZI VYENYE KEMIKALI

Kwa miaka mingi sasa, baadhi ya watu wamegubikwa na dhana potofu ya kwamba, kuwa mweupe ndiyo urembo .
Dhana hii imewafanya wengi waanze kutumia vipodozi vikali, bila kujali madhara ya baadaye.
Kwa mfano, hata baadhi ya wasanii, wake kwa waume, wamekuwa wakijibadili ngozi zao na tumewaona wakibadilika hatua kwa hatua.
Hata hivyo, unapohisi kuna uzuri, mara nyingi kuna kudhurika. Madhara ya awali ya vipodozi hivi, huonekana kwa mtumiaji kubabuka ngozi, kuwa na mabaka meusi au ngozi kuwa nyekundu. Lakini yapo madhara mengine mabaya zaidi ya hayo.
Kemikali hatari
Katika bidhaa hizo zinazotumika za kujichubua, kuna kemikali za aina mbili.
Kwanza ni ‘Hydroquinone’ na ya pili ni ‘Mercury’.
Hydroquinone kemikali hii ni sumu kali, ambayo hutumika kwa ajili ya kuchapisha picha na kutengeneza bidhaa za mpira.
Hutumika pia kama kisaidizi katika kutengeneza rangi za nywele.Mercury nayo ni kemikali ya sumu inayoweza kuuzwa katika maduka ya madawa tu tena bila maelekezo ya madaktari
linapokuja swala la afya zetu kwa siku hizi kumekuwa na mlipuko wa magonjwa mengi yasiyo kuwa na tiba na hii inachangiwa na vitu au vipodozi tunavyokua tunavitumia bila kujua nini chanzo chake na vina tengenezwa na nini, imefika  wakati watu k  lazima tujifunze na tuwe wasikivu sana hasa ujitabua na kuanza kutumia vipodozi asilia


MADHARA YATOKANAYO NA MATUMIZI YA VIPODOZI VYENYE VIAMBATO VYENYE SUMU
1.      BITHIONOL
athari zake.
Kupata mzio wa ngozi/allergic  na athari kwenye ngozi ikiwa itapata mwanga wa jua.

2.      HEXACHLOROPHENE
madhara/ athari
·  Inapenya kwenye ngozi na kuingia kwenye ishipa ya fahamu na kusababisha ugonjwa wa mishipa ya fahamu hasa kichwani.
·  Pia inasababisha ugonjwa wa ngozi na kuathirika kwa ngozi pindi unapokuwa kwenye mwanga wa jua.
·  Kwa watoto wachanga husababisha uhalibifu kwenye ubongo
·  Vile vile ngozi inakuwa laini na kusababisha kupata ugonjwa kama fangasi kwenye ngozi au maambukizi ya vimelea vya maradhi.



3.      ZEBAKI (MERCURY)
Madhara /Athari
·  Husababisha madhara ya ngozi, ubongo, figo na viungo, mbalimbali vya mwili
·  Zebaki inapopakwa kwenye ngozi kuweza kupenya taratibu ndani ya mwili na kusababisha sumu yake kuingia kwenye damu na kusababisha madhara mwengi mwilini.

Mama mjamzito akitumia vipodozi vyenye zebaki mtoto huathirika akiwa akiwa bado tumboni na huzaliwa akiwa na mtindio wa ubongo.
·  Husababisha ngozi kwa laini na kuwa na mabaka meusi na meupe
·  Husababisha mzio/ allergic wa ngozi na muwasho
·  Sumu iingiapo kwenye mishipa ya fahamu husababisha ugonjwa wa mishipa ya fahamu.
·  Sumu ya zebaki ikiingia mwilini kwa kiwango kikubwa husababisha madhara maka upofu, uziwi, upotevu wa fahamu wa madhara mara kwa mara.

Tuesday, November 3, 2015



Nguo Ndefu Ina Umuhimu Wake Kwa Mtoko Wa Usiku



NGUO fupi imekuwa maarufu kwa mitoko ya usiku kwa shughuli mbalimbali, na wadada wengi wamekua wakipendeza sana, lakini hata hivyo wengi wamesahau kuwa hata nguo ndefu ina umuhimu wake kiasi cha kufanya mavazi ya nguo fupi kwa usiku kama ndio utaratibu.

Ukitaka  kuchagua nguo ndefu kwa ajili ya mtoko wa usiku,  iwe ni sketi na blauzi,gauni,  suti nakadhalika, chagua yenye nakshi ambazo zitaendana na shughuli husika.

Unaweza pia kuchagua nguo ndefu ya kubana ama yenye mpasuo mrefu kidogo, na kiatu kirefu pia.

Uchaguzi wa nguo inayotakiwa kuvaliwa, kwanza  unatakiwa kuzingatia ambo mengi ikiwemo kuvaa kulingana na tukio husika, kama ni pati ya kawaida au ni kwa ajili ya sherehe fulani, uvaaji wako unatakiwa
kuzingatia rangi ya nguo na rangi ya mwili wako.

Kama wewe ni mweusi hutakiwi kuvaa nguo nyeusi kwani haitakupendeza, unashauriwa kuvaa nguo za rangi nyeupe,nyekundu, gold, bluu au njano.

 

Na kama wewe ni mweupe nguo ya rangi nyeusi au rangi nyingine itakupendeza kulingana na rangi ya ngozi yako.


Mfano wa nguo ndefu simple ya kutokea usiku

Nguo ndefu ni nzuri zaidi kama zitavaliwa kwa kiatu kirefu na kubeba wallet kubwa ama 'klatch.

Cha kuzingatia ni kuhakikisha kuwa nguo hiyo haikuletei tabu wakati wa kutembea kwani nguo ikiwa ndefu sana husababisha mvaaji kuishikilia na kuonekana wakati mwingine kama kituko, vaa nguo kulingana na umbo na hata urefu wako, nguo za wazi na ndefu hupendeza sana kama zitavaliwa
na mkufu au ushanga shingoni
.
Jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa, unakuwa na nguo maalum ya kutokea na unatunza vizuri nguo zako kwani hilo litakusaidia kuongeza umaridadi wako na kujiamini zaidi.

Lakini pia usisahau kuwa na vipuri vitakavyosaidia vazi lako. Faida ya vazi hili, si tu kupendeza na kuonekana maridadi bali  muda mwingine nguo ndefu hukufanya kuwa huru zaidi katika shughuli husika.